MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA CHOONI HUKO ENEO LA ALLY HASSAN MWINYI MJINI TABORA
Mwili
wa mtoto John Mwapwani (4) aliyefariki majira ya asubuhi baada ya
kutumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao mtaa wa Sikanda kata ya Chemchem eneo la
Ally Hassan Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora ukiwa unapandishwa kwenye gari la polisi.
Inasemekana kuwa mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi ,baba yake mzazi alimwambia
aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa
watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni.
Baada
ya kimya cha muda mrefu kutawala baba wa mtoto huyo alielekea sehemu
ya choo,lakini katika hali ya kusikitisha alikuta mwili wa mtoto huyo
ukielea kwenye maji machafu
akiwa tayari amepoteza maisha.
Picha na kapipij blog
0 comments: