HABARI MOTO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! MWANAUME AKAMATWA AKIWA UCHI AKIFUKUA KABURI - MPANDA

 
Na  Walter Mguluchuma,Mpanda Katavi
Mtu mmoja alitambulika kwa jina  la  Richald  Clavery  35  Mkazi wa Kijiji  cha Ikola  Tarafa ya Karema Wilaya ya Mpanda  anashikiliwa na jeshi la Polisi  baada  ya kukutwa  akifukua  kaburi la  marehemu aliyefahamika  kwa jina la  Tabu  Omera
Kwa mujibu wa  kaimu Kamanda wa Polisi  wa Mkoa wa Katavi   Francis Maro tukio  hilo lilitokea hapo Februari  22 majira ya saa nne usiku  kijijini hapo nyumbani kwa  Lenada  Sakafu ambae alikuwa ni dada wa marehemu huyo
Siku hiyo ya tukio  Lenada Sakafu  alikuwa nyumbani kwake  pamoja na majirani na ndugu na jamaa  zake wakiomboleza  msiba  wa mdogo wake marehemu  Tabu Omera  aliyekuwa amefariki Dunia  siku tatu kabla ya tukio hilo kutokana na kushindwa kujifungua nakuzikwa  nyumbani kwenye eneo la nyumba ya Lenada
Alifafanua kuwa   mtoto wa Lenada  aitwaye    Brandina  alitoka nje ya  nyumba kwa lengo la kwenda  chooni kujisaidia  ndipo aliposhituka kuona mtu akiwa anafukua kaburi la marehemu mama yake mdogo
Alisema hari hiyo ilimfanya Binti huyo arudi ndani ya nyumba na kutoa taarifa kwa mama yake pamoja na  majirani na ndugu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo
Watu  waliokuwa msibani hapo   walishitushwa na taarifa hiyo  nakulazimika kutoka nje ya nyumba  na waliweza  kumkuta  Richard   Clavery akiwa anafukua kaburi hilo la marehemu  Tabu huku akiwa   uchi  akiwa  amevua ngu zake zote  na kuzitundika kwenye msalaba  wa kaburi hilo
Kaimu kamanda  Francis Maro  alisema baada ya  watu hao kumuuliza anafanyanini hapo  ghafla mtuhumiwa alishituka  na akajifanya  kupandisha mashetani  hata hivyo watu hao waliokuwa msibani hawakujali walimkamata
Alisema   mtuhumiwa  anatajiwa kufikishwa mahakamani  ili aweze  kujibu  shitaka  la kufanya  kosa   la kufanya vitendo vya kishirikina.
 CHANZO - EDDY BLOG
 

0 comments:

MTOTO WA KIKE ABURUZWA NA BABA YAKE MTAA MZIMA KWENYE PIKIPIKI KWA KUSHINDWA KWENDA SHULE....!!!!



Mtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira.

Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
 
 Baada ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.

Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
 
Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.
Afisa upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa upelelezi zaidi.

Na Valence Robert-Geita

0 comments:

HIVI NDIVYO BASI LA BUNDA LINAVYOONEKANA BAADA YA KUGONGA TRENI KATIKA ENEO LA MANYONI MKOANI SINGIDA.....

MWENEKANI WA BASI LA BUNDA BAADA YA KUGONGA TRENI HUKO MANYONI MKOANI SINGIDA.


0 comments:

ENEO LA TUKIO AMBAKO BASI LA BUNDA LIMEGONGA TRENI NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU WANAOKADIRIWA KUFIKIA SABA NA WENYE ZAIDI YA 30 KUJERUHIWA VIBAYA......


Eneo la tukio ambako basi la bunda limegonga Treni huko Manyoni mkoani Singida.

0 comments:

HABARI MPASUKOOO!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! BUNDA BUS YAGONGA TRENI WATU SABA WASADIKIWA KUPOTEZA MAISHA NA WENGINE ZAIDI YA 30 KUJERUHIWA VIBAYA....

Habari kutoka wilayani Manyoni  mkoani Singida zinaeleza  kuwa Basi la Bunda lililokuwa linatoka Dodoma kuelekea Mwanza limegonga  Treni iliyokuwa inatoka Aghondi Itigi na kusababisha kifo vya abiria takribani saba na wengine zaidi ya thelathini kujeruhiwa vibaya.
 
Habari za awali zinasema kuwa  basi hilo limegonga kichwa cha treni hiyo.

Kwa taarifia zaidi na picha tutawaletea hivi punde kupitia mtandao huu…. 

0 comments:

MTOTO WA MIAKA MINNE AFARIKI DUNIA BAADA YA KUTUMBUKIA CHOONI HUKO ENEO LA ALLY HASSAN MWINYI MJINI TABORA

Mwili wa mtoto John Mwapwani (4) aliyefariki majira ya  asubuhi baada ya kutumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao mtaa wa Sikanda kata ya Chemchem eneo la Ally Hassan Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora ukiwa unapandishwa kwenye gari la polisi.
Inasemekana kuwa mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi ,baba yake mzazi alimwambia aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni.

Baada ya kimya  cha muda mrefu kutawala baba wa mtoto huyo alielekea sehemu ya choo,lakini katika hali ya kusikitisha alikuta mwili wa mtoto huyo ukielea kwenye maji machafu akiwa tayari amepoteza maisha.

Picha na kapipij blog 

0 comments:

WANAUUME WAMVUA NGUO MREMBO HADHARANI USIKU WA KUAMKIA LEO,ALIKUWA AMEVAA NUSU UCHI

Hapa ilikuwa ni pata shika ambapo dada huyo amewekwa kati huku vijana wa eneo hilo wakiwa wanapiga kelele huku wakimvua nguo na kumfanyia vitendo visivyo vya kibinadamu
 Anaeonekana kwa mbali ni mdada ambaye alijitolea kwenda kumsaidia dada huyo ambae alikuwa amevaa kanguo kafupi ka nusu utupu akikatiza maeneo kituo cha basi cha mwenge usiku huu
 Hapa akiwa amevuliwa nguo na baadhi ya kina mama kumsaidia na kumwingiza katika gari moja wapo ili kumsitili

 Umati wa watu ukiwa umeongezeka na kuzingira basi hilo la abiria na kudai ashushwe ili waweze kumchapa na viboko kwa kitendo cha kuwadhalilisha akina dada wengine 

NB-Hatukuweza kuweka picha za binti huyo akiwa mtupu kulingana na maadili.

Picha na Dar es salaam yetu 


0 comments:

MAMBA MLA WATU AUWA WAWILI NA KUJERUHI MMOJA - GEITA


 
Wananchi wa kijiji cha Nyansalala katika kata ya Bukondo wilaya ya Geita wameiomba serikali ya mkoa wa Geita kuwasaidia kumuua mamba anayewinda watu  na wanyama kando kando mwa ziwa Victoria.
Wakiongea kwa nyakati tofauti juzi wananchi hao wamesema  kuwa mamba huyo amewakosesha amani wananchi wa eneo hilo mpaka kufikia kuacha kufanya kazi   katika kjijij hicho hivyo kuiomba idara ya wanyamapori mkoa huo kuweza kumwinda na kumua.
 Diwani wa kata hiyo John Magulu amesema   kuwa kuna watu 2 wameuawa na mamba huyo na kuwataja waliouawa kuwa ni Luganga Lukana (30)  na mkazi wa kijijij cha Chankorongo  na  omary Amos (12) mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi Mapinduzi Bukondo.
Diwani huyo  amemtaja aliyejeruhiwa na mamba huyo kuwa ni kuwa ni Tizita Luhindisa   mkazi wa kijiji cha Kitigili katika kata hiyo(48) hivyo kuiomba serikali kuwasaidia kwa hali na mali wananchi wa vijiji hivyo.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza, diwani huyo amesema  pamoja na kupeleka taarifa kuhusu mamba huyo katika ofisi za wanyama pori wilaya ya Geita lakini hawajapata msaada wowote kutoka kwenye ofisi Aidha diwani huyo amewataka  wananchi hicho kushirikiana katika kuhakikisha wanamuua mamba huyo anayesumbua wananchi kila kukicha.

 Afisa wanyama pori wilaya ya Geita Bw Msese Kabulizina amekiri kuwepo kwa mamba huyo katika vijiji hivyo na kuongeza kuwa jitihada za kumuua mamba huyo zinaendelea kwa hali na mali kuweza kumpata na kuweza kumua na kuwaomba wananchi hasa wavuvi wanaovua kando kando ya ziwa kuwa makini na waangalifu wakati wa shughuli zao.
 

Na Valence Robert-Geita

 

0 comments:

CCM ni kibokooooo!!!!!!!!!!YAWANYAKUA MADIWANI WALIOJIUZULU CHADEMA SHINYANGA,NAPE AWAPOKEA MADIWANI HAO WA CHADEMA


Shamra shamra baada ya waliokuwa nmadiwani wa Chadema kuonekana katika eneo la mkutano wa CCM mjini Shinyanga
Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga mheshimiwa Gulam Hafiz Mukadam akishikana mkono na aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga bwana Sebastian Peter Mzuka maarufu kama Obama wa Ngokolo muda muchache baada ya kuwasili katika viwanja vya mahakama ya Mwanzo Nguzo 8 mjini Shinyanga katika mkutano wa katibu wa siasa na uenezi wa ccm taifa Nape Nnauye ,mkutano ambao wananchi wameouona kama ulikuwa na nia ya kuwapokea viongozi wa chadema Sebastiani Peter na Zacharia Mfuko wa kata ya Masekelo ambao kwa pamoja jana walifanya maamuzi ya kujivua udiwani wa kupitia tiketi ya CHADEMA.

Waliokuwa madiwani wa CHADEMA,kulia ni Sebastian Peter,aliyekuwa diwani wa Ngokolo katikati ni Nape Nnauye na kulia ni Zacharia Mfuko aliyekuwa diwani wa Chadema kata ya Masekelo wakiwa juu ya jukwaa kabla ya kuvua kombati zao na kurudisha kadi zao kisha kujiunga na CCM mbele ya Nape Nnauye jioni ya leo mjini Shinyanga

Sebastian Peter akikabidhi kadi ya CHADEMA kwa Nape Nnauye
Awali wakati wa mkutano wa hadhara wa Chama cha mapinduzi CCM jioni ya leo,Katibu wa siasa na uenezi CCM taifa Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara mjini Shinyanga katika viwanja vya mahakama ya mwanzo eneo la Nguzo Nane mjini Shinyanga.Kushoto ni mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini,ambaye pia ni naibu waziri wa madini Stephen Masele.
Aliyekuwa diwani wa Chadema Zacharia Mfuko juu ya jukwaa la CCM kama unavyoona amevaa kofia na skafu ya Chama tawala.
 Zacharia Mfuko akizungumza katika mkutano wa hadhara na kutangaza nia ya kuhamia CCM
Aliyekuwa diwani wa Chadema katika kata ya Ngokolo Sebastian Peter akizungumza katika mkutano wa CCM leo ambapo alisema ameamua kujiunga/kurudi nyumbani kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu yeyote na kukanusha habari zilizotapakaa mtaani kuwa yeye pamoja na mwenzake Zacharia Mfuko wamehongwa shilingi milioni 15 ili wahamie CCM.
 
Sebastian Peter akivua kombati na kuvua nguo za CCM

Viongozi mbalimbali akiwemo meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafiz Mukadam (wa kwanza kulia) na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga bi Anna rose Nyamubi pamoja viongozi wengine akiwemo katibu wa ccm mkoa na katibu wa siasa na uenezi CCM wakifuatilia  kwa umakini maneno ya wanachama wawili wapya Chama tawala CCM
Kombati za CHADEMA walizokuja wakiwa wamevaa wazivua na kuzichoma moto hadharani kama unavyoona zikiteketea kwa moto


Ndani ya gari la CCM Sebastian Peter na Zacharia Mfuko wakiondoka eneo la mkutano wameshavaa nguo za CCM kama unavyoona

Hili ndiyo gari waliyoondoka nayo wanachama hao wapya wa CCM katika eneo la mkutano mjini Shinyanga huku maswali mengi yakiendelea kubaki kwenye vichwa vya wananchi wa mkoa wa Shinyanga kuhusu maamuzi hayo waliyofikia kwa kukiona chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA si kitu tena pamoja na kwamba walikisifia kwa maneno matamu mwaka 2010 na kufanikiwa kupata kiti cha udiwani,lakini pia wengine kujiuliza kwanini wafanye vile wakati walikuwa wamebakiza muda mfupi tu kumaliza kazi waliyokuwa wamepewa na wapiga kura wao!!!

0 comments:

WAFANYAKAZI SHINYANGA KUFANYA MAAJABU SHEREHE ZA MEI MOSI 2014,FUATILIA HAPA KIKAO CHA WADAU WA MEI MOSI KILICHOFANYIKA MJINI SHINYANGA KUPANGA MIKAKATI YA KUCHANGIA SHEREHE HIZO KIMKOA


Katikati ni mwenyekiti wa Shirikisho  la vyama vya wafanyakazi TUCTA mkoa wa Shinyanga Bw. Fue Mrindoko akizungumza kwenye kikao cha wadau wa sherehe za  Mei Mosi mwaka 2014 mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Shinyanga ikiwa ni katika kuweka mikakati ya wafanyakazi mkoa wa Shinyanga kuchangia sherehe hizo.Mrindoko alisema katika mikakati ya kufanikisha sherehe hizo ambazo katika mkoa wa Shinyanga mwaka huu zitafanyika katika wilaya ya Shinyanga baada ya Kahama mwaka jana wamejipanga kikamilifu ili sherehe hizo ziwe za mfano wa kuigwa hapa nchini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bw. Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau wengi ambapo pamoja na mambo mengine alizitaka mamlaka zinazohusika na uaandaaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora zifanye kazi ya kuteua wafanyakazi bora kwa kuzingatia vigezo vinavyotakiwa lakini pia bila kuingiliwa na mtu wala mamlaka yoyote.Mkuu huyo wa mkoa alisema hatarajii ofisi yoyote kukosa mfanyakazi bora lakini pia akisisitiza vyombo vya habari kuwa ni wadau muhimu katika kufanikisha sherehe hizo muhimu kwa wafanyakazi

Katikati Mkuu wa mkoa akizungumza katika kikao hicho.Wa kwanza kulia ni kaimu katibu tawala msaidizi na rasiliamali watu wa mkoa wa Shinyanga bwana Kajia Godfey,wa pili ni katibu tawala mkoa bi Eva Loppa.Wa kwanza kushoto ni mratibu wa TUCTA mkoa wa Shinyanga,ambaye pia ni katibu wa chama cha wafanyakazi serikali kuu bi Tabu Mambo,akifuatiwa na mwenyekiti wa TUCTA mkoa wa Shinyanga Fue Mrindoko

Kikao kinaendelea,wa kwanza ni kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nhambaku ,akifurahia kitu ndani ya kikao hicho,wa pili ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson aliyekuwa mwenyeji wa sherehe za Mei Mosi mwaka jana 
Aidha kabla ya kilele cha sherehe hizo za mei mosi kutakufanyika michezo  mbalimbali kama vile mpira wa miguu,mpira wa pete,bao na karata,kuvuta kamba,kukimbiza kuku,riadha na mbio za baiskeli na michezo kadha wa kadha siku ya kilele cha sherehe hizo

 Mratibu wa TUCTA mkoa wa Shinyanga,ambaye pia ni katibu wa chama cha wafanyakazi serikali kuu bi Tabu Mambo akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema miongoni mwa wadau wa sherehe hizo ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi,wafanyakazi,waajiri pamoja serikali na siku ya sherehe za mei mosi zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wafanyakazi bora katika sekta binafsi na zawadi itaanzia shilingi 300,000/= na kuendelea,sekta za umma zawadi itaanzia shilingi 500,000/= na kuendelea,sekta ya migodi ya kati shilingi 500,000/= na kuendelea na sekta ya migodi ya mikubwa zawadi itaanzia shilingi 1,000,000/= na kuendelea
Awali akisoma taarifa ya wadau wa sherehe za Mei Mosi mwaka huu katika mkoa wa Shinyanga,katibu wa TUICO mkoa wa Shinyanga bwana Fabian Samkumbi (hayupo pichani) alisema wadau wa kuchangia sherehe hizo ni Vyama vya wafanyakazi kama vile TUGHE mkoa,CWT,TAWLGU,TPAW,TAMICO,CHODAWU,TUICO,CWT wilaya/Manispaa Shinyanga,CWT Kishapuna Kahama,RAAWU,TRAWU,TEWUTA,TTCL,COTWU.Wadau wengine aliwataja kuwa ni waajiri taasisi za serikali-TUGHE,wakurugenzi wa halmashauri za wilaya CWT,TUGHE na TALGU,wajiri wa sekta binafsi CWT,waajiri kutoka TAMICO,wajiri kutoka RAAWU,CHODAWU,TUICO,TPAWU,COWTU(T),TEWUTA na waajiri kutoka TRAWU
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Ukumbi huo wa mikutano ulikuwa umejaa sana tofauti na vikao vingine ambavyo hufanyika katika ukumbi huo
Ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia mawili matatu yaliyokuwa yanajiri katika kuhakikisha kuwa sherehe za mei mosi zinakuwa za mfano hapa nchini mwaka huu


0 comments:

PICHA ZA MADIWANI WALIONG'ATUKA CHADEMA MJINI SHINYANGA


Kushoto ni aliyekuwa diwani wa kata ya Masekelo bwana Zacharia Mfuko na kulia ni bwana Sebastian Peter Mzuka aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga ambao leo wamefanya maamuzi magumu kuachia ngazi na kubaki wanachama wa kawaida wa CHADEMA kwa kile walichodai kuchoshwa na siasa za chadema zilizojaa majungu na migogoro

0 comments:

POLISI LAWAMANI KWA KUJIHUSISHA NA WIZI - SIMIYU



MADIWANI katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani simiyu wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya maaskari wa jeshi la polisi wilayani humo kwa kuwapora raia mali na fedha zao pindi wanapoenda kuwakamata.


Read More »

0 comments:

Breaking News!! MADIWANI WAWILI WA CHADEMA WAJIUZULU NAFASI ZAO NA KUBAKI RAIA WA KAWAIDA SHINYANGA


Breaking News!! MADIWANI WAWILI WA CHADEMA WAJIUZULU NAFASI ZAO NA KUBAKI RAIA WA KAWAIDA SHINYANGA

Madiwani wawili wa Chama cha  Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  katika  manispaa ya Shinyanga wametanganza rasmi kujiuzulu nyadhifa zo kutokana na madai ya uongozi ngazi ya taifa  kuendelea kusikiliza majungu,kudhalilisha baadhi ya viongozi  pamoja na  kuwaita  wahaini au wasaliti katika chama  bila kuchambua ukweli na kutotekeleza waliyoyaahidi kwa wanachama wao.
Madiwani hao ni Sebastiani Peter (PICHANI) kutoka kata ya Ngokolo na Zacharia Mfuko kutoka kata ya Masekelo ambao wamedai  wanayatamka rasmi maneno  mbalimbali yaliyopelekea kujiuzulu kama inshara ya kuwajibika kwa niaba ya makosa yaliyofanywa na viongozi wa chama hicho kitaifa kwa nyakati tofauti.
HABARI KAMILI ITAKUJIA HIVI PUNDE KWANI WANGSTEVE BLOG IMEONGEA NA MADIWANI HAO NA INAENDELEA KUFUATILIA KWA UKARIBU ZAIDI SAKATA HILO KWA UNDANU ZAIDI....

0 comments:

DC BARIADI AWATAKA MADIWANI KUTOWAINGILIA WATENDAJI WA KATA



MKUU wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Bw. Erasto Sima amewataka madiwani wilayani humo kuacha kuwaingilia watendaji wa kata na vijiji wanaotekelza majukumu yao kwa kuwakamata wazazi waliokataa kuwapeleka watoto wao shule na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.


Read More »

0 comments:

CCM YAWANYEMELEA WALIOFUKUZWA CHADEMA KAHAMA



 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeanza mkakati wa kuwachukua waliokuwa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kahama waliofukuzwa uanachama hivi karibuni kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kumuunga mkono aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Zitto Kabwe.
 

Read More »

0 comments:

WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA WANAOONA POSHO HAITOSHI WAKAFANYE SHUGHULI NYINGINE. MWIGULU NCHEMBA

Wizara ya Fedha imepigilia msumari maombi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba ya kutaka waongezewe posho na kusema anayeona ameacha kazi inayomlipa zaidi kwenda bungeni afungashe virago na kuondoka.
Msimamo huo umekuja siku moja tu baada ya gazeti hili kudokeza kuwa madai ya wajumbe wa bunge hilo kutaka waongezewe posho kutoka Sh300,000 za sasa kwa siku, yamegonga mwamba baada ya kamati iliyoteuliwa kuchunguza uhalali wake kusema kiwango hicho kinatosha.
Mwenyekiti wa muda wa bunge hilo, Pandu Kificho alisema jana bila kutaja viwango, kuwa ripoti ya kamati hiyo imewasilishwa kwa Rais Jakaya Kikwete kwa uamuzi.
Madai ya wajumbe kutaka waongezewe posho, yamechafua hali ya hewa ndani na nje ya Bunge, huku baadhi ya wananchi wakipaza sauti zao na kumsihi Rais Kikwete alivunje bunge hilo iwapo wajumbe watashikilia msimamo wa kutaka nyongeza ya posho.
Jana, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba alisema wanaoshiriki kutunga Katiba ni Watanzania na siyo wataalamu washauri waliokodiwa kutoka nje.
Alisema kwa msingi huo, Serikali ilitarajia kuwaona watu hao wakitanguliza uzalendo zaidi badala ya kudai malipo manono.
“Katika kutengeneza Katiba hii, hatujakodi consultants (wataalamu washauri) kutoka Uingereza, Marekani, Kenya, Uganda wala nchi nyingine yoyote… Hawa ni Watanzania na kazi wanayoifanya ni yao,” alisema.
“Wangekuwa wataalamu wa kukodi wangeweza kudai malipo hayo, lakini hapa ni tofauti... wanafanya kazi yao na kila mtu anafanya kazi yake na anapaswa kujivunia kushiriki katika tendo hili la kihistoria kwa kutanguliza uzalendo,” alisema.
Nchemba alisema anazielewa hoja za baadhi ya wajumbe walioibua suala la posho, lakini kwa mtazamo wake, hoja hiyo hata kama ingekuwa na mashiko kiasi gani, imewasilishwa wakati usiokuwa mwafaka. Alisema wapo makandarasi na wazabuni waliotoa huduma kwenye taasisi mbalimbali za umma lakini hawajalipwa.
Alisema kwa kawaida, Februari ni mwezi mbaya kwa kuwa baadhi ya wilaya zina historia ya kukumbwa na uhaba wa chakula hivyo kuhitaji fedha nyingi za Serikali ili kuokoa maisha ya watu katika maeneo hayo.
Pia alisema si wakati mwafaka wa kudai nyongeza hiyo hasa ikizingatiwa kuwa kuna walimu wapya 30,000 nchini kote ambao hawajapangiwa vituo kutokana na kukosekana kwa fedha za kulipa stahiki zao.
Nchemba alisema mbali na walimu hao wapya kutokupangiwa vituo, walimu wengine wanadai malimbikizo ya fedha zao na kwamba hawajalipwa kutokana na ufinyu wa bajeti 
serikalini.
 Credit;googlehabari blog

0 comments:

SAKATA LA MASHINE ZA EFD,TRA YAWATOA HOFU WAFANYABIASHARA




Na Kenneth Ngelesi, Mbeya

MAMLAKA ya mapato nchini TRA imewatoa hofu wafanyabishara kutumia mashine za EFD kwani kodi inakatwa asilimia 30 ya faida baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji na manunuzi.


Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa juma na Afisa Mwandamizi Mkuu wa Elimu wa mamlaka ya Mapato nchini (TRA) makao Makuu Hamis Lepenza katika hotel ya Paridise jiji hapa katika Mkutano na waandishi kutoka vyombo mbalimbali ambao  uliyo itishwa na mamlaka hiyo kwa lengo la kuwataka wandishi wasaidie kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa mashine hizo.


Lupenza alisema kuwa hofu ya wafanyabiashara wengi kuto taka kutumia mashine hizo ni kuto kuwa tayari kukatwa asilimia hiyo ni kwamba wengi hawana elimu ya juu utumiaji wa mashine hizo.


Afisa huyo alisema kuwa wengi wao wamekuwa na malalamiko kuwa hawaja soma hivyo  kuwa nguma kwao kuzitumia miashine hizo jambo alilodai siyo la kweli bali ni janja ya wafanyabishara kwani wana hofia mashine hizo zitasababisha kuonyesha mauzo kuongezeka na kodi ya kulipa kuwa kubwa.


Aliongeza kuwa kutokana makato kuwa wazi katika ulipaji wa kodi ndiyo sabababu wafanyabiashara kutokuwa tayari kutuma mashine hizo.


Lepenzi alisema kuwa wafanyabishara wengi wamekuwa wakilala mika kuwa hawaja soma jambo hivyo uwezo wa kutumia msahine ni mgumu.


'Ndugu zangu huyu mfanyabishara anasema hajasoma hivyo hataweza kutumia mashine hizo lakini mtu huyo huyo unanunua simu nzuri kubwa na yenye mambo mengi kuliko hata hiyo mashine ya EFD' alisema Lupenza.


Aliongeza kuwa tatizo lingine lililopelekea zoezi kuwa gumu ni ugeni wa utamaduni wa kutumia mashine hizo katika jamii yetu na siyo kigezo cha elimu kama kinavyo tolewa na baadhi ya wafanyabishara walio wengi.


Katika hatau nyingine Afisa elimu na huduna ya mlipa kodi kutoka
makao Makao Makuu Sigsimund Kafuru aliwataka waandishi kusaidia kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhumu wa kudai risiti pindi wanapo nunua bidhaa kwani kutochukua risiti ni kuisosesha serikali mapato na hatimaye inashindwa kutoa huduma stahiki kwa wananchi wake.


Aidha Aliongeza kuwa ni vema wananchi wakajenga utamaduni wakudai risiti pindi wanapoa nunua bidhaa  yoyote ile.


Akijibu swali kwa waandishi habari sababu za kuteua makampuni kumi na moja tu kupewa jukuma na kusambaza mashine hizo kutokana na kushinda tenda baada ya kushindanisha kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.


Tangu mwaka 2010 serikali kupitia kwa mamlaka ya mapato nchi iliwatka wafanyabisha kutoa risiti  kwa kumtumia mashine hizo kwa sawamu ya kwanza ikianza na wafanyabisha lakini 200,000/ lakini mpka sasa bado kumekuwa na mvutano mkubwa baini ya ya Serikali na wafanya bishara hao.


Hata hivyo  zoezi hilo bado lina leta mvutano mamlaka hiyo imesema kuwa ipo katika mchakato wa kuanza kutoa hudumnu ya risiti kwa kutumia mashine hizo kwenye magari makubwa na mabasi ya kusafirishia abiria.

0 comments:

MILIPUKO YA MABOMU ZANZIBAR

 Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu cha mripuko katika eneo la Mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majera na na uharibifu wa majengo katika eneo hilo. 
 
 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa walipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo, wakati wa mripuko huo. 
Mkuu wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuangalia na kuchunguza tukio hilo la mripuko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu 
 
Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini, ikifuatia mlipuko uliotokea siku ya  Jumapili wiki iliyopita katika eneo la Pangawe. 
 
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa, isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana na matukio hayo.

Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi wakati huu hakuna mtu au mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na matukio hayo.
 
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo Kamanda Makame amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbali mbali visiwani humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa na amewaondoa hofu wananchi wa visiwa hivyo kuhusu usalama wao.

Chanzo: Zanz News$ bbc

0 comments: