ALIYETABIRI MWISHO WA DUNIA AFARIKI DUNIA
Mtume wa Kanisa
la World Message Last Warning nchini Uganda ambaye alitabiri kwamba mwaka 2000
utakuwa mwisho wa dunia, Wilson Bushara (53) amefariki dunia.
Bushara ambaye alivuta vyombo vingi vya habari
alipotabiri na kusisitiza kwamba mwisho wa dunia utakuwa Juni 30 mwaka
1999 na kushawishi waumini wake kuuza mali zao na kununua nafasi zao
mbinguni alifariki asubuhi ya jana.
Alitabiri na kusisitiza kwamba dunia itafikia mwisho wake kabla ya kuingia kwa milenia mpya, ambayo ilikuwa ni mwaka 2000.
Hata baada ya tarehe hiyo aliyoitaja kupita bila
tukio hilo kutokea, Bushara alikimbilia mafichoni baada ya polisi
kuvamia kambi yake ya maombi ya Bukoto iliyokuwa huko kwenye Wilaya ya
Luweero Jimbo la Nakaseke Septemba 18, 1999.
Bushara anatambulika kuwa ana ushirikiano na
kiongozi mwingine wa kundi la kidini, Joseph Kibwetere ambaye
aliwashawishi waumini wake zaidi ya 1000 kujichoma moto kanisani Machi
17, 1999.
Hata hivyo aliamua kukataa kuwa na ushirikiano na
Kibwetere pamoja na kuwa na ushahidi wa picha walizopiga kwenye matukio
kadhaa wakiwa pamoja.
Bushera pamoja na baadhi ya waumini wake ambao
wengi walikuwa wakifanya kazi za kuuza maziwa na uhudumu kwenye hoteli
wote walikimbilia wilayani Busia ambapo walijificha baada ya kusikia
taarifa kwamba polisi walikuwa wakitaka kuwakamata.
Alioa wake tisa aliokuwa akiishi nao kwa pamoja,
mmoja kati yao akiwa binti wa miaka 15.
Miaka 10 baadaye, yaani mwaka
2011 Bushara aliibuka na kutabiri kwamba dunia inaelekea kufikia mwisho
wake siku za karibuni na kuanza kugawa kadi za mwaliko kwa waumini wake,
kwa ajili ya tafrija maalumu ya “karamu ya mwisho” ambazo kila moja
iliuzwa kwa Sh23,000 za Uganda.
Aliwaeleza wafuasi wake kwamba ishara za mwisho
huo wa dunia ziko wazi ikiwemo miale mikali ya radi na milipuko ya
volcano wanayoishuhudia kwa mwaka huo ndiyo uthibitisho kwamba dunia
imefikia mwisho.
Kwa kusisitiza, aliwahakikishia kwamba wale watakaokuwa wamenunua kadi hizo ndio watakaopata fursa ya ‘kunyakuliwa’ moja kwa moja kwenda mbinguni na wale ambao hawatakuwa wamezipata, wataishia kwenye moto wa jehanamu.
Kwa kusisitiza, aliwahakikishia kwamba wale watakaokuwa wamenunua kadi hizo ndio watakaopata fursa ya ‘kunyakuliwa’ moja kwa moja kwenda mbinguni na wale ambao hawatakuwa wamezipata, wataishia kwenye moto wa jehanamu.
Kwa wakati huu, Bushara alikuwa makini akikataa
kutaja tarehe rasmi ya mwisho huo wa dunia aliokuwa akiutabiri. Bushara
amefariki huku akikabiliwa na mashtaka kadhaa mahakamani, ikiwemo
kufunguwa kanisa lake ambalo lilipigwa marufuku.
Mei mwaka jana alishtakiwa kwa ulaghai na kuitisha
mkusanyiko usiokuwa halali kisheria, kisha kushikiliwa kwenye gereza la
Luzira na hatimaye kuachiwa.
0 comments: