DC BARIADI AWATAKA MADIWANI KUTOWAINGILIA WATENDAJI WA KATA
MKUU
wa Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu Bw. Erasto Sima amewataka madiwani wilayani
humo kuacha kuwaingilia watendaji wa kata na vijiji wanaotekelza majukumu yao kwa kuwakamata wazazi
waliokataa kuwapeleka watoto wao shule na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwa
taarifa za baadhi ya madiwani kuwaingilia watendaji hao wa serikali ngazi za
vijiji na kata, pindi wanapokuwa watekeleza maagizo ya serikali.
Akiongea katika baraza la madiwani wa
halmashauri ya wilaya hiyo Mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa hatawavumilia
wanasiasa hao, wanaounga mkono wazazi wasiopeleka watoto wao shule, huku
akiwataadhalisha kuwa yeyote atakayebainika atamchukulia hatua za kishrei ikiwa
pamoja na kumkamata na kumweka ndani.
Ameeleza kuwa Wilaya ya Bariadi
mpaka sasa imeshindwa kufikia asilimia 70 ya watoto waliokwenda shule hasa wale
wanaotakiwa kuanza kidato cha kwanza, ambapo mpaka sasa kuna asilimia 30 tu ya
wanafunzi walioripoti kuanza kidato cha kwanza.
Pia
amewahimiza madiwani hao wanasimamia na kuhakikisha wanatekeleza maagizo ya
serikali na kufanya vikao vyote vya kisheria hasa vile vya maendeleo ya kata
(WDC) vinafanyika katika muda wake na kuhudhuliwa na majumbe wake wote huku
akisema kata za Sapiwi, Dutwa na Maubingi mpaka sasa zimeshindwa kufanya vikao
hivyo bila ya kutoa sababu maalumu.
0 comments: