MAMBA MLA WATU AUWA WAWILI NA KUJERUHI MMOJA - GEITA
Wananchi wa kijiji cha Nyansalala katika
kata ya Bukondo wilaya ya Geita wameiomba serikali ya mkoa wa Geita kuwasaidia
kumuua mamba anayewinda watu na wanyama kando kando mwa ziwa Victoria.
Wakiongea kwa nyakati tofauti juzi wananchi hao
wamesema kuwa mamba huyo amewakosesha amani wananchi wa eneo hilo mpaka
kufikia kuacha kufanya kazi katika kjijij hicho hivyo kuiomba idara
ya wanyamapori mkoa huo kuweza kumwinda na kumua.
Diwani wa kata hiyo John Magulu
amesema kuwa kuna watu 2 wameuawa na mamba huyo na kuwataja waliouawa
kuwa ni Luganga Lukana (30) na mkazi wa kijijij cha Chankorongo na
omary Amos (12) mwanafunzi wa darasa la 4 katika shule ya msingi Mapinduzi
Bukondo.
Diwani huyo amemtaja
aliyejeruhiwa na mamba huyo kuwa ni kuwa ni Tizita Luhindisa mkazi
wa kijiji cha Kitigili katika kata hiyo(48) hivyo kuiomba serikali kuwasaidia
kwa hali na mali wananchi wa vijiji hivyo.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza, diwani huyo
amesema pamoja na kupeleka taarifa kuhusu
mamba huyo katika ofisi za wanyama pori wilaya ya Geita lakini hawajapata
msaada wowote kutoka kwenye ofisi Aidha diwani huyo amewataka wananchi hicho kushirikiana katika kuhakikisha
wanamuua mamba huyo anayesumbua wananchi kila kukicha.
Afisa wanyama pori wilaya ya Geita Bw Msese
Kabulizina amekiri kuwepo kwa mamba huyo katika vijiji hivyo na kuongeza kuwa
jitihada za kumuua mamba huyo zinaendelea kwa hali na mali kuweza kumpata na
kuweza kumua na kuwaomba wananchi hasa wavuvi wanaovua kando kando ya ziwa kuwa
makini na waangalifu wakati wa shughuli zao.
0 comments: