MTOTO WA KIKE ABURUZWA NA BABA YAKE MTAA MZIMA KWENYE PIKIPIKI KWA KUSHINDWA KWENDA SHULE....!!!!
Mtoto Anastazia Jumanne akiwa amefungwa mikono yake kwenye pikipiki kwa mpira.
Mtoto Anastazia Jumanne (12) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya msingi katika wilaya na mkoa wa Geita amefanyiwa ukatili wa kutisha baada kufungwa mpira kwenye pikipiki na baba yake mzazi na kisha kuanza kumburuza mtaani.
Tukio
hilo la kusikitisha limetokea jana majira ya sa tatu asubuhi katika moja ya mitaa ya mjini humo ambapo inadaiwa kuwa binti
huyo anayesoma darasa la nne katika shule hiyo alikataa
kwenda shule kitendo ambacho kilimkasirisha baba yake aitwaye Jumanne
Nkoyogi ambaye pia ni mfanyabiashara wa samaki mjini Geita.
Mashuhuda
wa tukio hilo baada ya kuona asubuhi hiyo mtoto huyo akiburuzwa huku
amefungwa kwenye pikipiki walianza kupiga makelele na kukusanyana kwa
lengo la kumkamata baba huyo aliyekuwa anafanya unyama huo.
Baada
ya kumkamata na kumtia kumtia mikononi mwao walimpeleka kwenye ofisi ya sungusungu iliyopo
Ihayabuyaga kata ya Kalangalala na kufungiwa humo kwa usalama wake.
Akizungumzia tukio hilo katibu wa sungusungu kata ya Kalangalala aliyempokea
mtuhumiwa huyo Abel Richard alisema tukio hilo liliwafanya
wananchi kujaa jazba dhidi ya mzazi huyo na kutaka kumpiga.
Alisema mzazi huyo kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani Geita baada ya katibu huyo kuwasiliana na uongozi wa jeshi hilo na kuwatuma askari kwake kumchukua haraka kwa usalama wake.
Afisa
upelelezi wa mkoa wa Geita Simon Pasua amekiri kuwepo kwa tukio hilo na
kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi hadi sasa kwa
upelelezi
zaidi.
Na Valence Robert-Geita
0 comments: