vifo!!!!!!!!!!! WACHIMBAJI WADOGO WANANE WANADHANIWA KUFA KATIKA MACHIMBO YA NYANGALATA NA KALOLE WILAYANI KAHAMA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI.

 Baadhi ya Wachimbaji wadogo katika Mgodi wa Kalole wakihangaika kuwatoa wenzao wanane wanao daiwa kufariki dunia kwa kufukiwa na kifusi ndani ya shimo hilo.

 Wachimbaji Wadogo wakiaangalia sehemu walipofukiwa wenzao wakati wakichimba Dhahabu katika machimbo hayo madogo ya Kalole Wilayani Kahama.

 Haya ni baadhi ya Mashimo ambayo wachimbaji wadogo wamekuwa wakichimba katika Mgodi wa Kalole

 Mjiolojia kutoa Ofisi ya Afisa Madini Mkazi Wilyani Kahama Bw. Amir Chande akitoa maelekezo juu ya kufungwa kwa machimbo hayo baada ya maafa hayo kutokea
 Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kalole Bw. Furaha Mashamba akielezea juu ya kutokea kwa tukio hilo la maafa mbele ya Waandishi wa habari hawapo pichani.

 Mmoja wa Wachimbaiji katika Mgodi wa Kalole akiwa katika jitihada za kuwafukuwa wenzao wanaodaiwa kufukiwa katika machimbo hayo juzi
 Wachimbaji wadogo wa Kalole wakifuatilia kwa makini ufukuaji wa wenzao wanane wanaodaiwa kufia ndani ya mashimo walimokuwa wakichimba dhahabu yaliyofunikwa na kifusi kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo ya kanda ya Ziwa.

Majeruhi ambaye alisalimika katika tukio hilo akiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama akipatiwa Matibabu

0 comments: