POLISI LAWAMANI KWA KUJIHUSISHA NA WIZI - SIMIYU
MADIWANI katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani
simiyu wamelalamikia vitendo vinavyofanywa na baadhi ya maaskari wa jeshi la
polisi wilayani humo kwa kuwapora raia mali na fedha zao pindi wanapoenda
kuwakamata.
Wameyasema
hayo kwenye baraza la kawaida la madiwani wa halmashauri hiyo ambapo wamesema baadhi
ya maaskari wamekuwa sio waadilifu wa kazi na kujihusisha na vitendo vya wizi
na utapeli wakati wanapofanya doria usiku.
Diwani wa
kata ya Girya Bw. Safari Lewa amesema kumekuwepo na taarifa mbalimbali zinazolihusu
jeshi la polisi kuwa baadhi ya maaskari hasa wa usalama barabarani wamekuwa
wakiwatoza fedha baadhi ya madreva pikipiki bila kuwapatia stakabadhi kwa
kisingizio kuwa vitabu vimekwisha.
Almesema
wakati mwingine wamekuwa wakiwafukuza madereva wa pikipiki za abiria maarufu
kwa jina la bodaboda umbali mrefu hadi wakati mwingine huwasababishia ajali
pamoja na kuwachapa viboko na kuwatoza fedha kubwa ambayo katika mapato ya
serikali haiingizwi.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Bariadi Bw. Erasto Sima amelitaka jeshi la polisi
kupitia mkuu wa polisi wilani humo (OCD)J Bw. ulius Mjengi kuwachunguza baadhi
ya askari ambao wengi wao wanatuhumiwa na kashfa mbalimbali wanazozifanya.
Mkuu huyo pia
amemtaka OCD kukagua vitabu kwa askari wa usalama barabarani kuangalia mwezi
huu wameingiza kiasi gani cha fedha kama faini
kwa makosa mbalimbali ya vyombo vya moto kwa lengo la kutambua askari gani
anafanya kazi na haandiki risiti za malipo.
0 comments: