laana!!!!!!!!!!!! MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE ABAKW UCHOCHORONI, SOO LAMALIZWA KIFAMILIA!
WAKATI
asasi na taasisi mbali mbali zikiwemo TGNP, TAMWA na WRP zikipinga
vitendo vya ukatili wa kijinsia, hali hiyo imeonekana kutopewa mwitikio
na baadhi ya familia.
Kutopewa
kwa kipaumbele na kushindwa kuwachukulia hatua wanaofanya vitendo
hivyo kumetokana na Familia moja jijini Mbeya kutaka kumaliza kifamilia
suala la ubakaji lililotokea hivi karibuni.
Tukio
hilo lilitokea Machi 13 mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika Mtaa wa
Mapambano Kata ya Iyela wakati mtoto wa kike alipotumwa dukani na Mama
yake Mzazi na kukumbwa na tukio hilo.
Mtuhumiwa
wa tukio hilo ambaye ni mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Iyela
Jijini Mbeya Patrick Ndelwa(18) anatuhumiwa kumbaka Mwanafunzi wa darasa
la nne mwenye umri wa miaka nane(jina limehifadhiwa) shule ya Msingi
Mapambano Jijini Mbeya.
Hatua
ya kufikia wazazi wa pande zote mbili kutaka kumalizana kifamilia
imetokea baada ya Jeshi la Polisi kushindwa kufungua jalada la tukio
hilo tangu Machi 14, mwaka huu lilipolipotiwa.
Aidha
jalada la tukio hilo lilifunguliwa Machi 24 mwaka huu huku Polisi
wakitaka yafanyike mazungumzo katika pande hizo mbili na kushindwa
kuwachukulia hatua waliotenda makosa kama hayo.
Uchunguzi
umebaini kufanyika kikao Machi 26,mwaka huu eneo la Mapambano Iyela
kilichowakutanisha pande hizo mbili kwa nia ya kulimaliza nyumbani suala
hilo huku upande wa mtuhumiwa ukidai kuwa aliyetenda kosa hilo ni
yatima.
Aidha
imebainika kuwepo kwa mkakati wa kumhamisha mwathirika wa tukio hilo
kumpeleka Jijini Dar es Salaam kwa nia ya kupoteza ushahidi na Jalada
kutopelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali ili kukwamisha taratibu za
kumfikisha mtuhumiwa Mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Mama
Mzazi wa mwathirika wa tukio hilo,Salome Msigwa alisema aligundua
kubakwa kwa mwanae alipoanza kumuogesha Machi 13 mwaka huu majira ya saa
kumi na mbili jioni na alipomuuliza alijibiwa kuwa aliyembaka ni
Patrick Ndelwa ambapo alimtendea unyama huo katika kichochoro karibu ya
nyumba yao.
Alisema
baada ya kugundua tatizo la mtoto, alitoa taarifa kituo cha Polisi
ambapo mtuhumiwa alikamatwa na mtoto kupelekwa kupimwa Hospitali ya
Rufaa na kupewa Matibabu huku akitakiwa kufuatilia vipimo vingine Machi
28.
Baadhi
ya wadau wamelalamikia kuongezeka kwa vitendo ya ukatili dhidi ya
watoto na kwamba vimekuwa vikiongezeka Jijini Mbeya sehemu kubwa imekuwa
ikichangiwa na Dawati la Kijinsia la Jeshi la Polisi kutokana na
kugeuka Mahakama kuyamaliza matatizo kwa kupatanisha pande
zinazotuhumiana.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amekiri kupokea tatizo hilo kwamba jeshi lake linafanyia uchunguzi suala hilo likikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi amekiri kupokea tatizo hilo kwamba jeshi lake linafanyia uchunguzi suala hilo likikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
VIA- PAPARAZI
0 comments: