mchezo mchafu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!DIWANI WA CCM KATA YA KALANGALALA AKAMATWA NA KADI FEKI ZA CHADEMA,ZIKIWA NA SAINI YA MBOWE
Kadi feki za CHADEMA zikiwa na saini ya mwenyekiti wa CHADEMA taifa Freeman Mbowe |
Diwani wa viti maalumu wa Chama cha
Mapinduzi kata ya Kalangalala na tarafa ya Geita wilayani Geita mkoani Geita Zaitun Sued Fundikira anayeishi katika mtaa wa Mission amekamatwa na kadi za kugushi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Kadi zilizogushiwa ni 23 zikiwa na saini ya mwenyekiti
CHADEMA taifa Freeman Mbowe,kadi ambazo hazijaandikwa chochote katika baadhi ya
sehemu kama vile jina la mwanachama na sehemu anayokaa.
Wakisimulia juu ya tukio hilo mashuhuda walisema kuwa
mnamo saa nne asubuhi alitokea mtoto mmoja akiwa na kadi za Chadema amezishika
mkononi akitembea nazo mtaani na kutokeza katika kijiwe cha Kalakana ya
wakereketwa wa Chadema maarufu kama “Kijiwe
cha Sengerema” ndipo walipomuona mtoto huyo walipomuuliza akasema kuwa amezitoa
ndani kwani zimo nyingi sana.
Mara baada ya kuambiwa hivyo wakamwambia mtoto huyo
awapeleke na mtoto huyo aliongozana nao hadi nyumbani kwa diwani huyo na walipofika
,mtoto aliingia ndani na kuwaletea kadi nyingi mkononi huku akiwa na mkoba
umejaa kadi zingine.
Muda mchache tu baada ya mtoto kutoka na kadi hizo
huku wakereketwa hao wakizichukua ghafla diwani huyo alijitokeza nje huku
akihaha na kufoka kuwa hizo kadi hazijui.
“Nashangaa mimi
kadi hizi sizijui kabisa licha ya kuwa kwenye mkoba wangu lakini sijui nani aliyeziweka
humu,na mwandishi yeyote atakayeniandika nitamshtaki’’,alieeleza diwani huyo.
Taarifa za kuaminika kutoka kwa wananchi wamesema kuwa
diwani huyu amekuwa akiratibu shughuli mbalimbali za kutaka kudhoofisha Chadema
katika eneo hilo ambapo inadaiwa kuwa hadi kombati za Chadema zimeshaandaliwa
ikiwa ni pamoja na kadi hizo feki kwa ajli ya kuhakikisha ujio wa aliyekuwa
naibu katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe atakapokuja kanda ziwa wapewe watu
kadi hizo na kuvulishwa kombati za chama ili watamke kuwa wamejitoa Chadema.
Mwenyekiti wa mtaa wa mission anakoishi diwani huyo wa viti maalum,Juma
Kajala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Baadhi ya watu wamesema kuwa diwani huyo amekuwa
akiratibu mambo mengi lakini cha ajabu wamemshangaa kugushi hadi sahihi za
mwenyekiti wa CHADEMA taifa wakati mwenyekiti taifa hagawi kadi .
Uchunguzi umebaini kuwa hata ndani ya chama cha
mapinduzi mtoa taarifa amesema kuwa diwani huyo aliwahi kuteuliwa kuwa katibu
wa jumuiya ya wanawake wilayani Geita lakini baadae uteuzi wake ulisitishwa
mara moja baada ya kubaini kuwa mienendo yake siyo mizuri hivyo hadi CCM
walishamshtukia.
Naye kaimu katibu wa mkoa wa Chadema Rogers Luhega
alisema kuwa wa tayari taarifa hizo wameshazipeleka katika kituo cha polisi
Geita na kufungua jalada la mashitaka kwa ajili ya kumshitaki diwani
huyo.
Na Valence Robert- Geita.
0 comments: