Masikitiko!!!!!!!!!!!!!!!!!! ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUCHINJWA NA BABA YAKE HUKO KAHAMA MKOANI SHINYANGA.

   Mtoto Said Siraji akiwa amelazwa katika Hospital ya wilaya ya Kahama.

MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika shule ya msingi Majengo wilayani Kahama mkoani Shinyanga Said Joshua (12) amenusurika kufa baada ya kuchinjwa kwa kutumia kisu na baba yake mzazi kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa kumtibu mtoto maradhi yanayomsumbua.

Tukio hilo limetokea jana saa 11.00 alfajiri katika kijiji cha Majengo ,kata ya Majengo,tarafa ya Kahama mjini ambapo mwanamme aitwaye Joshua Salvatory(37) mkazi wa eneo akiwa nyumbani kwake alimkata kisu shingoni mtoto huyo na kuathiri koromeo lake.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya wilaya Kahama Dkt. Joseph Fwoma amesema mtoto huyo alifikishwa hospitalini hapo baada ya kuokotwa na wasamaria wema huku akivuja damu nyingi shingoni.

Amesema baada ya mtoto huyo kufikishwa hospitalini madaktari walimfanyia upasuaji na kumshona sehemu ya koromeo alilochinjwa na hali yake inaendelea vizuri hasa baada ya kuongezwa damu.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo Bi. Mariamu Idd (35) amesema, mtoto wake alichukuliwa na baba yake mzazi siku moja kabla ya tukio hilo na  kwenda naye kwake mitaa ya Majengo kwa kuwa waliksinsha achana naye na kudai kuwa alimchukua kwenda kumtibu kutokana na tatizo lake la kiafya ambalo hakulitaja.

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo,ambapo,kamanda wa  polisi mkoa wa Shinyanga SACP Evarist Mangalla alisema chanzo cha tukio hilo kinasadikiwa kuwa mtuhumiwa anadhaniwa kuwa na matatizo ya afya ya akili.

PICHA - MALUNDE1 BLOG

 

 


0 comments: