noma sana!!!!!!!!!! MBONGO NA WANAIGERIA WATATU WAKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA DAR.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova.
Raia raia watatu wa Nigeria na Mtanzania mmoja wamekamatwa jijijini Dar
es Salaam wakitaka kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya
mamilioni shilingi.
Watu hao walikamatwa Machi 18 mwaka huu saa 8:30 mchana katika ofisi za kampuni inayosafirisha mizigo ya kimataifa (DHL) zilizopo mkabala na Mliman City wakiwa na dawa hizo katika kifurushi ambacho ndani yake kilikuwa na vitabu vitatu, kila kimoja kikiwa na dawa za kulevya aina ya heroine zinazokadiliwa kuwa na ujazo wa nusu kilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova (pichani) alisema watu hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwenda nchini Liberia, Afrika Magharibi.
Kova aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, watuhumiwa walipohojiwa walisema waliamua kutumia mbinu hiyo kusafirisha dawa hizo kutokana na serikali kudhibiti njia zilizokuwa zimezoeleka.
Alisema uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea kufanyika ili kubaini thamani halisi, ujazo pamoja na kuthibitisha aina ya dawa hiyo baada ya Mkemia Mkuu wa serikali kukamilisha taratibu zake.
Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi limewakamata watu wawili wenye asili ya Kiasia wanaojihusisha na vitendo vya utekaji nyara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujipatia fedha.

0 comments: