Tanzia!!!!!!!!!! KIBOKO AMUUA MVUVI UFUKWENI MWA ZIWA VICTORIA AKIVUA SAMAKI.
Mwanaume
mmoja, Mukoba Juma mkazi wa Kijiji cha Guta B wilayani Bunda mkoani
Mara ameshambuliwa na kuuawa na Kiboko katika ufukwe wa Ziwa Victoria
wakati akifanya shughuli za uvuvi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Guta B, Kisheri Nyihande amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo na kusema kuwa juzi saa 12 jioni marehemu pamoja na rafiki yake
aliyemtambulisha kwa jina moja la Madege walienda kuvua katika ziwa
Victoria kwa lengo la kupata kitoweo.
Nyihande alisema wakiwa katika shughuli hiyo ghafla alijitokeza mnyama huyo na aliyemrusha marehemu ndani ya maji huku yeye Madege akitimua mbio kunusuru maisha yake.
Nyihande alisema wakiwa katika shughuli hiyo ghafla alijitokeza mnyama huyo na aliyemrusha marehemu ndani ya maji huku yeye Madege akitimua mbio kunusuru maisha yake.
Alifafanua
kuwa Madege alipiga kelele kitendo kilichowafanya wananchi kufika
katika eneo la tukio na kuanza kuutafuta mwili wa marehemu ambao hata
hivyo ulipatikana jana saa tatu asubuhi ukiwa na majeraha makubwa na
mwili huo kuzikwa jana saa 10 jioni.
Wakiwa
katika eneo la mazishi huku wakiwa na majonzi mengi wananchi
wakiungana na familia ya marehemu waliomba serikali kupitia kitengo cha
maliasili kuweka mkakati wa kudumu wa kufanya doria katika maeneo hayo
ili kunusuru maisha ya wananchi hao.
Mtendaji
wa Kijiji hicho Reymond Misana alisema tayari katika siku za hivi
karibuni wakazi watatu wa kijiji hicho wamepoteza maisha kwa
kushambuliwa na wanyama hao hasa Mamba na Kiboko na wengine kupata
ulemavu.
Aidha alisema fidia au kifuta jasho kwa familia zinazoathiriwa na wanyama hao imekuwa kitendawiili licha ya serikali ya kijiji kuwasilisha malalamiko hayo kwa idara ya mali asili wilayani Bunda.
0 comments: